Tazara yaanza kuingiza treni binafsi kwenye reli yake - bongoresults Tazara yaanza kuingiza treni binafsi kwenye reli yake - bongoresults
Business

Tazara yaanza kuingiza treni binafsi kwenye reli yake

Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) leo Machi 20 2024 limesaini makubaliano na kampuni ya Bravo Group ya Tanzania kwa ajili kutumia Njia ya Reli ya TAZARA kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Zambia, Congo, Zimbabwe na South Africa.

Tazara imeingia makubaliano hayo kama sehemu ya utekelezaji wa azimio la mageuzi ya kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji kupitia reli ikiwa Tanzania ni miongoni mwa Mataifa ulimwenguni yenye uhitaji mkubwa wa usafirishaji wa bidhaa zinazoingia nchini kupitia Bandari ambapo kuingia kwa bidhaa hizo kunatoa mianya ya kuhitajika usafirishaji kwenda nchi jirani.

Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA, Eng. Bruno Tadeo Ching’andu amesema kuwa makubaliano haya yataboresha zaidi biashara ya reli ya TAZARA, na anaona kutakua na biashara kubwa zaidi ukilinganisha na biashara waliyonayo kwa sasa.

Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Bravo Group, Bi. Angelina Ngalula amesema anashukuru juhudi za Mheshimiwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Tanzania inakua kitovu cha usafirshaji mizigo kwa ukanda wa SADC.

Bi Ngalula amesema  ‘Mipango hii ingeanza muda kidogo toka 2021 bahati mbaya miundombinu ya TAZARA haikua rahisi kwa kampuni nyingine kuingiza treni, Kwa sasa tutaanza na treni 2 ambazo zitakua zinapishana, treni moja itakua na jumla behewa 20 na kila behewa litabeba tani 50 ambapo jumla tani 1,000 sawa na malori 40 zitabebwa kwa pamoja, na kwa ujumla treni hizi mbili ni sawa na lori kubwa 80, Kadri TAZARA watakavyoongeza njia sisi tutaingiza treni nyingi zaidi’ – Ngalula.

Top Stories, TZA HABARI 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top